TIHEST

TIHEST

TASO na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu

TANDABUI STUDENTS ORGANISATION (TASO) KUTEMBELEA WATOTO WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU

SERIKALI YA TASO kwa ushirikiano na wanafunzi pamoja na UONGOZI WA CHUO, tarehe 24/12/2022 imefanikiwa kuwatembelea WATOTO wanaoishi kwenye MAZINGIRA MAGUMU na YATIMA wanaolelewa na kituo cha watoto kiitwacho CHRIST’S HOPE INTERNATIONAL kilichopo BUGARIKA CENTER MWANZA.

Kwenye hafla hii serikali ya TASO ikiongozwa na Rais wake Mhe, ENOCK P. HIMU iliambatana na msafara wa viongozi akiwemo Madam FRIDA Mwadili (Dean) wa wanafunzi akiwa Kama mwakilishi wa uongozi wote wa Chuo, Mhe, Makamu wa Rais Mr. MULEE KAURA, Katibu mkuu kiongozi, Mhe. ERICK O. FELIX, Mhe. Speaker wa Bunge – TASO Mhe, FLORIAN RWENYAGILA, Mhe, MARCO JILALA- Waziri wa Afya na viongozi wengine,

Aidha SERIKALI YA TASO kwa ushirikiano na wanafunzi pamoja na UONGOZI WA CHUO CHETU TUMEFANIKIWA KUWAPELEKA WATOTO HAWA VITU vifuatavyo;

UNGA wa Ngano 25kg mfuko mmoja (1).
Mafuta ya kupikia Lita 10, Ndoo moja (1).
Mchele kilo 40Kg na maharage kilo 10Kg
Daftari za msomi 200 sawa na katoni 2.
Kalamu Za Wino Box 1, SABUNI Za Unga na Miche, nguo aina mbalimbali za kike kwa kiume, unga LISHE.
Aidha SERIKALI YA TASO inapenda kuwashukuru Sana Wanafunzi wote kwa ushirikiano wenu katika kufanikisha Jambo hili, Asanteni kwa michango na ushiriki wenu.

Shukran za dhati kwa Mh, AMINIEL SHANGALI Mkuu wa chuo Tandabui, Mr. Shaibu Chanzi Campus Coordinator na uongozi wote wa Chuo chetu Cha TANDABUI kwa mchango wenu pia katika kufanikisha Jambo hili.